TENDERS AREA
Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila inawatangazia kuwa,kutakuwa na mnada wa hadhara tarehe 07/12/2024 (Jumamosi) saa 4:30 asubuhi ,utakaofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila kwa ajili ya kuuza mali mbalimbali zilizotumika ambazo ni :
1.Vifaa mbalimbali vya ofisi na mali mbalimbali kama; viyoyozi, vifaa vya umeme, vyuma chakavu, meza, fremu za milango ya mbao, fremu za milango ya chuma, madirisha, na mali nyingine nyingi
2.Vifaa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Hospitali
MASHARTI YA MNADA:
1.Mnunuzi atatakiwa kulipia kiasi chote cha bei iliyofikiwa siku ya mnada kwa mali zote zitakazonunuliwa kwa bei chini ya milioni moja (1,000,000/=). kwa mali zitakazouzwa kwa bei zaidi ya milioni moja, mteja anaruhusiwa kulipa kiasi chote cha pesa kwa mkupuo au kulipa asilimia ishirini na tano (25%) siku ya mnada na kiasi kinachobaki ndani ya siku kumi na nne(14).
2.Mali zitakaguliwa siku ya Alhamisi tarehe 05/12/ 2024 kuanzia saa 4:00 asubuhi au siku ya mnada. Gharama zinazohusiana na ukaguzi kama usafıri ni za mnunuzi mwenyewe.
3.Mnunuzi ataruhusiwa kuchukua mali baada ya kukamilisha malipo yote yanayaostahili.